Afrika Kusini yatangaza kikosi chake

Imebadilishwa: 5 Novemba, 2012 - Saa 15:25 GMT
Bafana Bafana

Kucheza dhidi ya Zambia tarehe 14 Novemba 2012

Timu ya taifa ya soka ya Afrika Kusini, imetangaza kikosi chake ambacho kitapambana na Zambia katika mechi ya kirafiki.

Afrika Kusini imeamua kuwaalika wachezaji wake nchini Ubelgiji, Darren Keet na Anele Ngcongca katika mechi hiyo dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambai.

Pambano hilo litachezwa tarehe 14 mwezi Novemba.

Keet ni kati ya walinda lango wawili wa timu hiyo, naye mlinzi wa timu ya Genk, Ngcongca, amechaguliwa kwa mara ya kwanza na kocha wa timu ya taifa, Gordon Igesund.

Kufuatia Steven Pienaar kustaafu kutoka mechi za kimataifa, mlinzi wa zamani wa Tottenham ya Uingereza, Bongani Khumalo, sasa ataiongoza timu hiyo kama nahodha.

Wachezaji wa Afrika Kusini wanaocheza soka nchini Uingereza, Kagisho Dikgacoi na Dean Furman, pia wamo katika kikosi hicho chenye wachezaji 24.

Mechi hiyo itachezewa katika uwanja wa FNB mjini Johannesburg, na itatumiwa na makocha wa timu zote mbili kujipima nguvu katika hali ya kujiandaa kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, mashindano ambayo yatafanyika Afrika Kusini.

Michuano hiyo itafanyika kati ya tarehe 19 Januari hadi tarehe 10 Februari mwaka 20113.

will likely be used by both coaches as an important preparation for next year's Africa Cup of Nations which takes place in South Africa.

Igesund alisema: "Hii huenda ikawa ni nafasi ya mwisho kwa wachezaji wa timu zote mbili, hasa wale wanaocheza ng'ambo, kung'ara uwanjani."

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.