Vilabu vingi vinamtaka Beckham

Imebadilishwa: 20 Novemba, 2012 - Saa 15:28 GMT
David Beckham

David Beckham

Klabu ya Paris Saint-Germain ni miongoni mwa vilabu maarufu duniani ambavyo vimeonyesha nia ya kumsajili David Beckham.

Beckham mwenye umri wa miaka 37, ametangaza kuwa atakihama klabu ya Los Angeles Galaxy, baada ya kandarasi yake kukamilika mwezi Desemba mwaka huu.

Tayri mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England, amepokea ombi kutoka kwa vilabu kadhaa nchini Urussi, Uchina, Australia na Brazil.

Ripoti zinasema, kuwa Beckham atakubali kandarasi na klabu yoyote ikiwa atatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wake 11 wa kwanza.

Beckham, anaripotiwa kutumia muda uliosalia kabla ya kumalizika kwa mkataba wake kujadili uwezekano wa kusaini mkataba na klabu nyingine.

Je Beckham atasajiliwa na klabu ipi?

Klabu ya PSG ilimpa Beckham kandarasi ya mamilioni ya paundi Novemba mwaka uliopita, lakini alikataa kusaini kandarasi hiyo kutokana na sababu za kifamilia.

Lakini baada y kuiongoza klabu ya LA Galaxy, kushinda kombe la ligi kuu kwa mara ya pili nchini Marekani, Beckham anahisi kuwa ni wakati muafaka kwake kuondoka.

Vilabu kadhaa nchini Brazil na Urussi zimetangaza azma yao ya kutaka kumsajili Beckham, lakini habari ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa mchezaji huyo kwa sasa anachunguza uwezekana wa kucheza nchini Uchina.

Klabu moja kutoka Afrika Kusini pia imeonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo, lakini huenda ikashindwa kutokana na malipo ya mchezaji huyo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.