Mark Huges afutwa kazi

Imebadilishwa: 23 Novemba, 2012 - Saa 11:26 GMT
Mark Hughes

Mark Hughes

Kocha wa QPR, ambayo kwa sasa iko mkiani kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier ya England Mark Hughes amefutwa kazi.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo, kocha huyo amefutwa kazi kutokana na matokeo mabaya tangu kuanza kwa msimu huu.

Baada ya mechi 12 kuchezwa QPR haijashinda hata mechi moja.
Taarifa hiyo imesema kuwa, bodi hiyo inajadili mipango ya kutangaza wasimamizi wapya wa klabu hiyo muda mfupi ujao.

Mark Bowen na Eddie Niedzwiecki watasimamia klabu hiyo wakati wa mechi ya ya kesho Jumamosi dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford.

''Bodi ya wakurugenzi ingependa kutoa shukrani kwa Mark, kutokana na juhudi zake wakati alikuwa kocha wa klabu hiyo kwa muda wa miezi kumi iliyopita'' taarifa hiyo iliongeza.

Wakurugenzi hao wamesema watangaza mipango mipya ya klabu hiyo muda mfupi ujao na aliyekuwa kocha wa Tottenham Harry Redknapp anatarajiwa na wengi kuteuliwa kuwa kocha mpya wa QPR.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.