Redknapp atazamiwa kuiokoa QPR

Imebadilishwa: 24 Novemba, 2012 - Saa 20:32 GMT

Harry Redknapp, kama meneja, aliitizama timu yake mpya ikichezea ugenini, ilipopata bao la kwanza lakini Manchester United katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford ilifanikiwa kuishinda Queens Park Rangers 3-1.

Harry Redknapp

Mashabiki wa QPR wana imani Redknapp ataweza kuwaokoa kusalia katika ligi ya Premier

QPR, ambayo Jumamosi ilimtangaza Redknapp kama meneja wake mpya, ilipata nafasi ya kuongoza katika mechi hiyo wakati Jamie Mackie alipofunga akiwa hatua chache kutoka lango.

Magoli ya kichwa kutoka kwa Jonny Evans na Darren Fletcher yaliweza kuinyanyua Man United.

Kwa muda wa saa nzima, Manchester United hawakucheza kama walivyotazamia mashabiki wengi, lakini kufuatia magoli matatu katika kipindi cha dakika nane, mambo yalibadilika kabisa.

Mchezaji wa zamu Javier Hernandez alifunga bao la tatu, na kuwawezesha vijana wa Sir Alex Ferguson kurudi kileleni katika ligi kuu ya Premier.

Shinikizo sasa ni kwa majirani Manchester City, ambao wakitaka kurudi kileleni itabidi sasa wajitahidi kuwashinda Chelsea katika mechi ya Jumapili.

QPR, ambao walimfuta kazi Mark Hughes siku ya Ijumaa, bado wanavuta mkia katika ligi, na mpaka sasa hawajapata ushindi katika mechi yoyote msimu huu, baada ya kucheza mechi 13.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.