Gold atoa onyo kali

Imebadilishwa: 27 Novemba, 2012 - Saa 12:37 GMT
David Gold

David Gold

Mmiliki wa Klabu ya West Ham, mwenye asili ya Kiyahudi David Gold, amesema klabu hiyo itachukua hatua kali dhidi ya mashabiki wake ambao watapatikana na hatia ya kutumia lugha ya Ubaguzi au kuonekana kufanya vitendo vinavyoashiria ubaguzi wa rangi.

Mashabiki wawili wa klabu hiyo tayari wamepewa onyo na polisi na mmoja wao amepigwa marufuku ya kutohudhuria mechi zote za West Ham maishani baada ya vitendo vyake wakati wa mechi yao na Tottenham siku ya Jumapili.

Gold alisema ''tuna sheria kali dhidi ya vitendo vyovyote vinavyoashiria ubaguzi na klabu hii haiwezi kuvumilia vitendo hivyo.''

''West Ham ni klabu ambayo inahimiza uvumilivu na utengamano wa watu kutoka jamii zote, bila kuzingatia misingi ya kabila au dini'' aliongeza Gold.

Mlinda lango wa West Ham kutoka Israel, Yossi Benayoun, amesema alihuzunishwa sana na matamshi na vitendo vya mashambiki hao wakati wa mechi hiyo.

Shirikisho la mchezo wa soka nchini Uingereza FA, limesema kuwa litafanya uchunguzi baada ya mashabiki kadhaa wa West Ham kutuhumiwa kufanya vitendo vinavyowadhihaki mashabiki wa Tottenham ambao wana uhusiano wa karibu na Wayahudi.

Tottenham ilishinda mechi hiyo 3-1.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.