Grant harudi Chelsea

Imebadilishwa: 3 Disemba, 2012 - Saa 14:44 GMT
Avrant Grant

Avrant Grant

Chelsea imekanusha madai kuwa kocha wake wa zamani Avram Grant, anarejea tena kumsaidi kocha wa sasa Rafael Benitez.

Benitez hajashinda mechi hata moja tangu aliposajiliwa wiki chache zilizopita, baada ya Roberto Di matteo kufutwa kazi.

Magazetti kadhaa nchini Uingereza zimeripoti kuwa, Grant ambaye aliongoza Chelsea hadi fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya mwaka wa 2008, atasajiliwa kama mmoja wa washauri wa kiufundi.

''Hakuna ukweli wowote kuhusu madai kuwa Avrant Grant atarejea tena katika klabu ya Chelsea'' alisema msemaji wa klabu hiyo.

Mashabiki wa Chelsea walighadhabishwa sana na uamuzi wa wasimamizi wa klabu hiyo wa kumfuta kazi Di Matteo na mahala pake kuchukuliwa na kocha wa zamani wa Liverpool, Rafa Beneitez.

Benitez kwa sasa anakabiliwa na shinikizo chungu nzima, kufuatia kipigo cha magoli kwa matatu kwa moja walichopewa na klabu ya West Ham siku ya Jumamosi.

Katika mechi zingine Chelsea ilitoka sare ya kutofungana bao lolote na Manchester Citu na Fulham.

Grant, 57, anaenziwa sana na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich na amekuwa kocha hur tangu alipojiuzulu kama kocha wa klabu ya Partizan Belgrade mwmezi Mei mwaka huu.

Grant aliongoza Chelsea, kuanzia Septemba mwaka wa 2007 bada ya Jose Mourinho kuondoka licha ya kuongoza Chelsea kushinda ligi kuu ya Premier kwa miaka miwili mfululizo, lakini alifutwa kazi baada ya Chelsea kushindwa kwenye fainali za kombe la mataifa bingwa barani ulaya na Manchester United kupitia mikwaju ya Penalti.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.