Nemanja Vidic hoi kwa jeraha

Imebadilishwa: 5 Disemba, 2012 - Saa 14:16 GMT

Nahodha wa Manchester United Nemanja Vidic ana jeraha la goti

Nahodha wa Manchester United Nemanja Vidic hatarejea uwanjani, kufuatia jeraha katika mechi ya ligi ya klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Cluj.

Vidic, 31, hajacheza tangu kufanyiwa upasuaji wa goti mwezi Septemba lakini alikuwa ameratibiwa kucheza leo dhidi ya Waromania hao.

Lakini sasa mlinzi huyo hatashiriki mechi hiyo na pia hatakuwepo Jumapili katika "Manchester Derby."

Wayne Rooney ataanza katika kikosi tofauti sana, baada ya United kufuzu kama viongozi wa kundi H.

Mkufunzi wa Manchester United Alex Ferguson alisema: " Sidhani Vidic atacheza. Anahisi anahitaji siku zingine kadhaa za mazoezi.

"Hatacheza katika derby iwapo hatacheza kesho, licha ya kuwa sikutarajia kumshirikisha Jumapili.

" Tutawapumzisha baadhi ya wachezaji lakini lazima tutende haki kwa timu zote zinazotarajia kufuzu kwa michuano tofauti- iwe ni katika ligi ya klabu bingwa barani Ulaya au Kombe la Uropa.

" Kwa hiyo tutachezesha kikosi kitakachotarajiwa kushinda. Lakini kutakuwa na mabadiliko."

Ferguson pia amethibitisha kuwa mchezaji wa kimataifa wa Japan Shinji Kagawa amerejelea mazoezi na ana nafasi finyu ya kushiriki katika mechi ya mwishoni mwa juma.

Kikosi kinachotarajiwa: Lindegaard, De Gea, Rafael, Jones, Smalling, Wootton, Ferdinand, Buttner, Evra, Cleverley, Giggs, Fletcher, Powell, Scholes, Carrick, Young, Hernandez, Welbeck, Rooney, Van Persie.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.