Ferguson afurahia ushindi

Imebadilishwa: 10 Disemba, 2012 - Saa 14:06 GMT
Kocha wa Manchester United

Kocha wa Manchester United akizungumza na waandishi wa habari

Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson, ametaja ushindi wao wa mabao 3-2 dhidi ya mahasimu wao wa jadi, majirani na mabingwa watetezi Manchester City, kuwa ushindi muhimu katika harakati zao za kutwaa kombe hilo msimu huu.

Mkwaju wa Robin van Persie, katika muda wa ziada wa mechi hiyo iliipa Manchester ushindi huo na pia kumaliza rekodi ya Manchester City ya kutoshindwa katika mechi 37 nkatika uwanja wao wa nyumbani.

United imesalia kileleni mwa ligi hiyo la alama 39, sita mbele ya Manchester City.

Ferguson amesema ushindi wao ulikuwa muhimu sana kwa kuwa ilikuwa ni mechi ya 31 ya ligi ya premier kati ya timu hizo mbili.

''mechi hiyo ilikuwa ngumu sana. Na hilo linaashiria kuwa viwango vya soka katika ligi kuu vimeimarika kwa kiasi kikubwa'' alisema Ferguson.

Robin Van Persie aipa United ushindi

Robin Van Persie

Robin Van Persie na Wayne Rooney wakisherehekea bao lao

Kabla ya mechi hiyo, Manchester City haiukuwa imepoteza mechi yoyote katika uwanja wao wa Etihad, tangu tarehe 20 Desemba mwaka wa 2010, wakati waliposhindwa na Everton.

Kufikia wakati wa mapunziko, United ilikuwa ikiongoza kwa mabo mawili kwa bila, magoli yaliyofungwa na Wayne Roonet.

Lakini katika kipindi cha Pili, Yahya Toure akaizawazishia Mancheter City.

Dakika chache kabla ya mechi hiyo kumalizika, kwaju wa Robin Van Persie ulimgusa Pablo Zabaleta na kutikisa lango la Manchester City na hivyo kuwapa vijana hao wa Sir Alex Ferguson ushindi huo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.