FA kuanzisha uchunguzi

Imebadilishwa: 10 Disemba, 2012 - Saa 14:00 GMT
Rio Ferdinand

Rio Ferdinand baada ya kujeruhiwa na shabiki mmoja wa Manchester City

Afisa mkuu mtandaji wa Chama cha wachezaji wa kulipwa wa soka, nchini Uingereza Gordon Taylor, amesema huenda ikahitajika kujenga ua unaozunguka uwanja ili kuwalinda wachezaji.

Taylor aliyasema hayo baada ya tukio la siku ya Jumapili, ambapo shabiki mmoja aliingia uwanjani na kumshambulia mchezaji wa Manchester United, Rio Ferdinand, wakati walipokuwa wakisherehekea bao lililofungwa na Lionell Messi, dhidi ya mahasimu wao wa Jadi Manchester City.

''Mimi nadhani hili ni jambo ambalo tunapaswa kuliangalia zaidi, imependekezwa kuwa ua ujengwe kuuzunguka uwanja hasa katika maeneo yaliyo wazi'' alisema Taylor.

Mashabiki nao wakataa pendekezo hilo

Aliongeza kuwa ujenzi huo unaweza kuwa karibu na maeneo ya goli au karibu na bendera iliyoko katika kila pembe ya uwanja.

Joe Hart

Kipa wa Manchester City akimzuia shabiki kumshambulia Rio Ferdinand

Ferdinand alionekana kuvuja damu kutoka usoni baada ya shabiki mmoja kurusha sarafu uwanjani na kumgonga karibu na macho.

Licha ya Ferdinand kupuuzilia mbali tukio hilo, shirikisho la mchezo wa soka nchini Uingereza FA limesema limeanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo, ambalo pia limekemewa vikali na wasimamizi wa Manchester City.

Kipa wa Manchester City, Joe Hart, alilazimika kumzuia shabiki mmoja, ambaye alikuwa ameingia uwanjani kutomkaribia Ferdinand, ambaye alikuwa anajaribu kuzuia uso wake kutokana na maumivu.

Lakini mwenyekiti wa chama wa mashambiki wa soka nchini Uingereza, Malcom Clarke, amesema uamuzi wa kujenga ua unaozunguka uwanja sio suluhisho la tatizo hilo.

''Ujenzi wa ua sio jambo ambao tunahisi ni wazo nzuri kwa sasa'' alisema Bwana Clarke.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.