Masaibu ya QPR yanaendelea

Imebadilishwa: 12 Disemba, 2012 - Saa 15:16 GMT
Adel Taarabt

Adel Taarabt mchezaji nyota wa QPR

Adel Taarabt amesema ataamua msimu wa Krismasi ikiwa ataichezea Morocco wakati wa michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwezi ujao nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo amesema uamuzi wake utategemea ikiwa klabu yake ya Queen Park Rangers itaandikisha matokeo mema katika mechi za ligi kabla ya michuano hiyo.

Kwa sasa klabu ya QPR imo mkiani kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier ya England, na wakati huo kuandikisha rekodi ya kuwa klabu ya kwanza katika historia ya ligi kucheza mechi Kumi na Sita vila ushindi wowote na Taarabt amedokeza kwua kocha wake amemuuliza kutoshiriki katika fainali hizo nchini Afrika Kusini.

''ni uamuzi mgumu sana. Kwa sasa, ninatarajia kucheza kadri ya uwezo wangu nikiwa na klabu yangu kabla ya muda huo kufikia wa kuchukua maamuzi. Lakini naafikiria kuwa nitashiriki'' Alisema TaarabT.

Harry Redknapp atakubali kumuachilia?

Harry Redknapp

Harry Redknapp kocha wa QPR, akiwa akitoa ushauri kwa wachezaji wake

Mchezaji huyoi mwenye umri wa miaka 23, amesema alishauriana na kocha wake Harry Redknapp, siku ya Jumatatu, kujadili fainali hizo zitakazochezwa nchini Afrika Kusini, baada ya kufahamishwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Morocco Rachid Taoussi anamtaka kujiunga na kikosi chake maarufu kama Atlas Lions.

Mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham, ambaye amecheza mechi Kumi na Mbili msimu huu, na kufunga magoli mawili, amesema nia yake kuu ya kuichezea timu hiyo ya taifa ya Morocco, lakini anakubali kuwa anakabiliwa na uamuzi mgumu, kwa sababu itamaanisha kuwa atakosa mechi tano za ligi kuu ya premier na klabu yake inayotishia kuondolewa kwa ligi kuu.

Mchezaji mwingine wa QPR Samba Diakite amesema yuko tayari kusalia na timu yake baadala ya kuakilisha Morocco katika mashindano hayo ya Afrika.

Taarabt anasema ni wakati mwafaka kwa shirikisho la mchezo wa soka barani Afrika CAF, kuandaa mashindano hayo kila baada ya miaka miwili, sawa na mashindano ya bara ulaya, ili kutoa nafasi kwa kwa wachezaji wengi wanaocheza katika ligi mbali mbali kushiriki.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.