Chelsea yashindwa na Corinthians 1-0

Imebadilishwa: 16 Disemba, 2012 - Saa 15:19 GMT
Mchezaji wa Corinthians

akisherehekea bao lake dhidi ya Chelsea

Klabu ya Corrinthians kutoka Brazil, imeshinda kombe la klabu bingwa duniani baada ya kuilaza Chelsea bao moja kwa bila katika mechi ya fainali iliyochezwa nchini Japan.

Paolo Guerrero aliifungia Corinthians, bao hilo muhimu na la ushindi.

Hata hivyo Chelsea, ilipoteza bafasi nyingi za kufunga wakati wa mechi hiyo.

Katika muda wa ziada Fernando Torres, alipoteza nafasi nzuri sana ya kuzawazisa licha ya kuwapiku walinzi wa Corinthians na kubakia kipa pekee.

Torres alijaribu kumchenga kipa wa Corinthians lakini kombora lake likawa hafifu na kudakwa kwa urahisi na kipa.

Chelsea ilimaliza mechi hiyo ikiwa na wachezaji kumi baada ya Gary Cahil, kupewa kadi nyekundu baada ya kumfanyika madhambi mchezaji wa Corrinthians Emerson.

Bao la chelsea lililofuingwa kwa kichwa na Fernando torres lilikataliwa na hivyo vijana hao kutoka brazil wakaibuka na ushindi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.