Kocha wa Harambee Stars ajiuzulu

Imebadilishwa: 17 Disemba, 2012 - Saa 18:50 GMT
Henri Mitchel

Aliyekuwa kocha wa Kenya

Kocha wa Harambee Stars Henri Michel amejiuzulu miezi minne tu baada ya kusaini mkataba na shirikisho la mchezo wa soka nchini Kenya FKF.

Kocha huyo kutoka Ufaransa, amekuwa kwenye mgomo baridi baada ya FKF kutomlipa mshahara wake wote.

Michel hulipwa shillingi milioni nne na manaibu wake wawili nao hupokea mshahara wa milioni moja unusu.

Kwa mujibu wa barua kutoka kwa Ubalozi wa Ufaransa mjini Nairobi kocha huyo anarejea nyumbani hii leo.

Hata hivyo barua hiyo inaashirikia kuwa kocha huyo alijiuzulu tarehe kumi mwezi huu lakini tangazo hilo limetolewa leo tarehe 17 Desemba.

Michel alikataa kuongoza Harambee Stars wakati wa michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA, akiitaja mashindano hayo kama mashindano yasiyokuwa na maana yoyote.

Henri Mitchel

Aliyekuwa kocha wa Kenya Henri Mitchel

Kocha huyo alisema jukumu lake kuu ni kuhakikisha Kenya imejianda vyema kwa michuano ya kuwania ubingwa wa mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi ya nyumbani.

Awali rais wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Kenya Sam Nyamweya alikariri kuwa kocha huyo alikuwa na jukumu la kuandaa Harambee Stars kwa michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka wa 2014.

Michel aliongoza Harambee Stars katika mechi mbili pekee. Katika mechi ya Kwanza Harambee stars ililazwa magoli 2-1 na Bafana Bafana ya Afrika Kusini mjini Nairobi na pia kulazwa 1-0 na Kilimanjaro Stars ya Tanzania.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.