Walcott hajaafikiana lolote na Arsenal

Imebadilishwa: 18 Disemba, 2012 - Saa 16:00 GMT
Kocha wa Arsenal

Arsene Wenger kocha wa Arsenal

Arsene Wenger amekariri kuwa Arsenal inamatarajio makubwa ya kutatua mzozo kuhusu kandarasi na mchezaji wake Theo Walcott, na kumshawishi mshabulizi huyo wa timu ya taifa ya Uingereza kusaini mkataba mpya.

Walcott scored alifunga bao wakati wa mechi ya siku ya Jumatatu usiku ambapo Arsenal iliilaza Reading kwa magoli 5-2, na kuoyesha amza yake ya kucheza katika nafasi ya tisa.

Mchezaji huyo anakamilisha kandarasi yake na Arsenal mwisho wa msimu huu na vilabu vya Chelsea, Liverpool na Manchester United vimeonyesha nia ya kumsajili mechazaji huyo.

''Sio uamuzi wangu, ni uamuzi ambao Theo Walcott pia anastahili kuamua'' Alisema Arsene Wenger.

Theo Walcott

Theo Walcott akisherehekea baada ya kufunga bao

"Naamini kuwa amepata masomo na klabau ya Southampton na Arsenal na kwa sasa amekuwa mmoja wa wachezaji wazuru sana. Natarajia kuwa wakati atakapoamua hatma yake, ataipa Arsenal nafasi ya kwanza'' Aliongeza kocha huyo.

Walcott alisajiliwa kutoka kwa klabu ya Southampton akiwa na umri wa miaka 16 mwaka wa 2006 kwa kitita cha pauni milioni tano na kupanda hadi pauni milioni kumi na mbili nukta tano na maefunga jumla ya magoli 52 baada ya kucheza mechi 237 na klabu ya Arsenal.

Duru zinasema kuwa ikiwa atakubali kandarasi mpya Walcott atalipwa kitita cha pauni elfu Sabini na Tano kwa wiki lakini hakuna makubaliano yoyote ambayo yameafikiwa.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.