Mashabiki wakataa wachezaji weusi-Urussi

Imebadilishwa: 18 Disemba, 2012 - Saa 14:46 GMT
Wachezaji wa Zenit

Wachezaji wa Zenit ya Urussi

Mashabiki wa klabu ya Zenit St Petersburg inayoshiriki katika ligi kuu ya premier nchini Urussi, wametoa wito kwa wasimamizi wa klabu hiyo kutowasajili wachezaji weusi na wale wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Kundi kubwa zaidi la mashabiki wa klabu hiyo maarufu kama ''Landscrona'' limesema kuwa klabu hiyo limelazimishwa kuwasajili wachezaji weus.

Wamesema, wachezaji ambao wanashiriki katika mapenzi ya jinsia moja, ni aibu kwa mji wao ambo una heshima zake.

Lakini mkurugenzi wa klabu hiyo wa masuala ya michezo, Dietmar Beiersdorfer,amesema wachezaji wa klabu hiyo husajiliwa bila kuzingatia mahala au nchi wanakotoka,rangi au dini wanayoshiriki.

Hata hivyo klabu hiyo ya Zenit, imethibitisha kuwa inafahamu umuhimu wa uvumilivu.

Hadi mwanzo wa mwaka huu, klabu ya Zenit ndiyo iliyokuwa klabu ya pekee inayoshiriki katika ligi kuu ambayo haikuwa na mchezaji mweusi.

Mapema mwaka huu klabu hiyo Zenit walimsajili mshambulizi Hulk kutoka Brazil na mcheza kiungo kutoka Ubelgiji Alex Witselfor kwa kitita cha pauni milioni 64.

Mcheza kiungo cha wa Ufaransa Yann M'Vila aliripotiwa kukataa uhamisho hadi klabu hiyo mwezi Agosti mwaka huu kutokana madai ya ubaguzi wa rangi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.