Wenger ateta bodi ya wakurugenzi

Imebadilishwa: 20 Disemba, 2012 - Saa 15:11 GMT
Arsena Wenger

Kocha wa Arsenal Arsena Wenger

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema amekuwa akiungwa mkono na bodi ya klabu hiyo nyakati zote

Mfanyabiashara maarufu kutoka Uzbekistan Alisher Usmanov, ambaye ndiye mwenye hisa wa pili anayemilikia asilimia kubwa ya hisa za klabu hiyo amesema Wenger hapati kuungwa mkono vilivyo na bodu ya wakurugenzi wa klabu hiyo na pia kushutumu vikali hatua ya kumuuza nyota wake Robin van Persie kwa klabu ya Manchester United.

Kampuni ya Red & White Holdings inayomilikiwa na mfanyabiashara huyo haina mwakilishi katika bodi ya wakurugenzi.

Lakini wenger amesema'' Naamini nimekuwa nikipata msaada kutoka kwa bodi na ninafurahia hilo''

Mapema wiki hii Jack Wilshere, Alex Oxlade-Chamberlain, Kieran Gibbs, Carl Jenkinson na Aaron Ramsey walisanini mikata mipya na muda mrefu na klabu hiyo.

Wenger hana nia ya kuwasajili wachezaji wapya

Wenger pia anamatrajia makubwa kuwa mshambulizi matata wa timu ta taifa ya Uingereza Theo Walcott atasaini mkataba mpya na klabu hiyo.
Kandarasi ya Walcott inakamilika mwisho wa msimu huu.

Hata hivyo, fedha zilizotengwa na klabu hiyo kwa matumizi ya kuwasajili wachezaji wapya na mishahara, ilibanawa na bodi ya klabu hiyo wakati Arsenal ilipohama kutoka uwanja wake wa zamani wa Highbury hadi uwanja mpya wa Emirates mwaka wa 2006.

Licha ya hayo yote Arsenal ilichapisha vitabu vyake vya hesabu vilivyoonyesha kuwa mapato yake yaliongezeka mwaka wa 2012 na pia kupata ufadhili wa pauni milioni mia moja hamsini kutoka kwa shirika la ndege la Emirates.

Wenger anaamini kuwa sera ya klabu hiyo ya kujitosheleza na fedha wanazopata hatimaye itaanza kuzaa matunda siku zijazo.

Hata hivyo kocha huyo amekaririm kuwa kutumia fedha nyingi kuwasajili wachezaji mwezi ujao, haitakua jambo la busara kwa klabu hiyo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.