Man United kucheza na Real Madrid

Imebadilishwa: 21 Disemba, 2012 - Saa 10:52 GMT
Sir Alex Ferguson na Jose Morinho

Sir Alex Ferguson na Jose Morinho

Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson anaamini kuwa mechi yao dhidi ya Real Madrid katika raundi ya pili ya michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya, ndiyo mechi kubwa na ngumu zaidi.

Timu hizo mbili hazijakutana tangu mwaka wa 2003 wakati zilipopepetana katika robo fainali ya michuano hiyo mechi ambayo Real Madrid ilishinda kwa magoli 6-5.

Cristiano Ronaldo, atakuwa akirejea katika uwanja wa Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu aliposajiliwa na Real mwezi Juni mwaka wa 2009, kwa kitita cha pauni milioni 80.

Mechi hiyo itatoa fursa kwa Ferguson, kurejelea uhasama wake na kocha Jose Mourinho.

Makocha hao wawili hawajakutana, tangu Manchester United ilipoondoa Inter Milan katika kinyang'anyiro hicho katika hatua ya robo fainali mwaka wa 2009.

Manchester United imeratibiwa kuchuana na mabingwa wa Uhispania Real Madrid katika uwanja wa Old Trafford.

Celtic itacheza na mabingwa wa Italia Juventus, Arsenal kupepetana na Bayern Munich ya Ujerumani.

Mabingwa mara nne wa kombe hilo Barcelona kucheza na mabingwa mara saba wa kombe hilo AC Milan nayo Valencia kutoa udhia dhidi ya Paris St Germain.

Borussia Dortmund imepangiwa kucheza na Shakhtar Donetsk, Porto kutoana jasho na Malaga, ili hali Galatasaray kucheza na Schalke 04.Mechi za awamu ya kwanza zitachezwa kati ya tarehe 12 au 13 au tarehe 19 au 20 mwezi Februari na mechi za marudiano imepangiwa kuchezwa kati ya tarehe 5 -6 au 12-13 mwezi Machi mwaka ujao.

Droo Kamili

Galatasaray vs FC Schalke

Celtic vs Juventus

Arsenal vs Bayern Munich

Shakhtar Donetsk vs Borussia Dortmund

AC Milan vs Barcelona

Real Madrid vs Manchester United

Valencia vs Paris St Germain

FC Porto vs Malaga

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.