Tanzania yaifunga Zambia 1-0

Imebadilishwa: 22 Disemba, 2012 - Saa 18:20 GMT
Tanzania wakimenyana na Zambia jijini Dar es Salaam

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imeilaza timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo kwa bao moja kwa bila katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa katika uwanja wa taifa mjini Dar es Salaam, Tanzania.

Katika mechi hiyo bao pekee la washindi, lilipatikana sekunde chache kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza likitiwa kimiani na mshambuliaji Mrisho Ngassa.

Timu ya Zambia, ambayo ni mabingwa wa Afrika ikiwa pia timu bora ya mwaka barani Afrika na yenye mchezaji bora wa mwaka wa BBC, Christopher Katongo, ilitawala mpira kipindi cha kwanza lakini ikokosa umakini katika umaliziaji.

Kwa upande wa timu ya Tanzania, ambao walionekana kutojiamini katika kipindi hicho, taratibu walibadilika, na kumiliki sehemu ya kiungo.

Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto,Frank Domayo na Salum Abubakar waliichosha ngome ya Zambia kwa kuelekeza mashambulizi mengi, langoni mwa Chipolopolo.

Mrisho Ngassa kama angekuwa makini zaidi angeweza kuipatia timu yake bao la mapema zaidi.

Timu ya Zambia ilichezesha nyota wake wengi akiwemo Christopher Katongo na Stopila Sunzu ambaye anatarajiwa kujiunga na timu ya Reading ya England.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.