Ameobi akataa kucheza fainali za Afrika

Imebadilishwa: 24 Disemba, 2012 - Saa 16:37 GMT
Shola Ameobi

Shola Ameobi mchezaji wa Newcastle

Mshambulizi wa Newcastle United Shola Ameobi amesema kuwa hatashiriki katika michuano ya kuwania Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika na timu ya taifa ya Nigeria.

Haya ni kwa mujibu wa kocha mkuu wa klabu hiyo Allan Pardew.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza ya vijana wasiozidi umri wa miaka 21, ametajwa katika kikosi kitakachoakilisha Nigeria katika fainali hizo zitakazo andaliwa nchini Afrika Kusini.

Kocha wa Nigeria Stephen Keshi amesema ana mataumaini makubwa kuwa mchezaji huyto atabadili uamuzi huo na kujiunga na timu hiyo kabla ya kuelekea nchini Afrika Kusini.

Lakini Pardew amesema mchezaji huyo mwenye umri wa maika 31, hataweza kushiriki katika fainali hizo za Afrika zitakazoanza tarehe kumi na tisa Januari.

Ameobi alizaliwa katika eneo la Zaria, Kaskazini mwa Nigeria kabla ya kuhamia Uingereza kuishi na wazazi wake akiwa na umri wa miaka mitano.

Victor Moses

Victor Moses mchezaji mwingine aliyepewa idhini na FIFA kuichezea Nigeria

Chini ya sheria za FIFA wachezaji ambao wameakilisha taifa moja katika mashindano ya vijana chipukizi anaweza kuichezea timu ya taifa lingine ikiwa atatimiza masharti yaliyowekwa

Ameobi alijumuishwa katika kikosi cha Super Eagles miaka kumi iliyopita lakini alikataa kujiunga nalo akisema nia yake ilikuwa ni kuichezea timu ya taifa ya Uingereza.

Mchezaji huyo hata hivyo alipewa kibali na shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA kuichezea taifa lake mwezi uliopita pamoja na mchezaji wa Chelsea Victor Moses.

Alicheza mechi yake ya kwanza na Super Eagles mwezi uliopita wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Venezuella ambapo Nigeria ilishinda kwa magoli matatu kwa moja.

Nigeria imo katika kundi la C na itacheza na mabingwa watetezi Zambia, Ethiopia na Burkina Faso katika mechi za raundi ya kwanza.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.