Gerrard kuendelea kuichezea Liverpool

Imebadilishwa: 24 Disemba, 2012 - Saa 13:47 GMT
Steve Gerrard

Naodha wa Liverpool Steve Gerrard

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amesema anataka kuongeza muda wa kandarasi ya nyota wake Steven Gerrard ambaye pia ni naodha wa klabu hiyo akisema kuwa mchezaji huyo bado angali na majumu mengi katika kalbu hiyo.

Mkataba wa Gerrard na Liverpool unamalizika mwisho wa msimu ujao na kocha huyo anasema bado anataka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka thelathini na mbili kuendelea kuichezea klabu hiyo.

Mcheza kiungo huyo wa England amefunga magoli 153 baada ya kuichezea Liverpool mechi 609.

Gerrard alisajiliwa na Liverpool mwaka wa 1998 na aliiongoza klabu hiyo kushinda kombe la klabu bingwa barani Ulaya mwaka wa 2004-05.

Naodha huyo pia aliiongoza Liverpool kushinda komeb ha FA mara mbili, kombe la ligi mara tatu na kombe la EUFA.

Gerrard amecheza mechi zote la Ligi tangu kocha mpya wa klabu hiyo Brendan Roggers kuteuliwa mwanzo wa msimu huu, na amefunga bao katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Aston Villa na Fulham.

Mwaka wa 2004, Steve Gerrard alikata kukihama klabu hiyo, ikiwa na pamoja na mpango wa Chelsea wa kumsajili mwaka wa 2004.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.