Ligi ya England kuendelea Kesho

Imebadilishwa: 25 Disemba, 2012 - Saa 12:17 GMT
Mashabiki wa Manchester United

Mashabiki wa Manchester United

Vinara wa ligi kuu ya Premier ya England kwa sasa Manchester United inajiandaa kuendelea uongozi wao wakati watakapoialika Newcastle hiyo Kesho.

Mabingwa watetezi Manchester City nao watakuwa nyumbani kucheza na Sunderland.

Katika mechi zingine, Reading inayoshikilia nafasi ya mkia imepangiwa kucheza na Swansea, West Brom nayo kusafiri ugenini kupepetana na QPR.

Baada ya kuandikisha matokeo yasiyoridhisha katika mechi yao ya mwishoni mwa juma lililopita, Manchester United itakuwa ikipania kujiimarisha kileleni mwa ligi hiyo kwa kuandikisha ushindi.

United ilitoka sare mechi yao ya mwisho dhidi ya Swansea na kufikia wakati huu bado imo alama nne tu mbale ya mabingwa hao watetezi.

Vilabu hivyo viwili vilipoteza mechi zao za tarehe 26 Desemba msimu uliopita uliopita na makocha Alex Ferguson na Roberto Mancini tayari wametoa onyo kwa wachezaji wao kuzuia matokeo kama hayo.

Baada ya kuandikisha ushindi wa magoli manane kwa yai dhidi ya Aston Villa, Chelsea imeratibiwa kucheza na Norwich.

Liverpool kutoana jasho na Stoke city na Fulham kualika Southampton katika uwanja wao wa nyumbani wa Craven Cottage.

Mechi kati ya Arsenal na West Ham imehairishwa kutokana na uwezekano wa kuwepo kwa mgomo wa madereva wa treni.

Totten kuchuana na Aston Villa na Everton kucheza dhidi Ya Wigan.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.