Ferguson azozana na Pardew

Imebadilishwa: 28 Disemba, 2012 - Saa 14:49 GMT
Sir Alex Ferguson

Sir Alex Ferguson

Kocha wa Manchester Sir Alex Ferguson amemshutumu kocha wa Newcastle Allan Pardew na kumtaja kuwa mfarisayo na mnafiki.

Pardew alimshutumu Ferguson kwa utovu wa nidhamu baada ya mechi yao siku ya jumatano.

Pardew amesema shirikisho la mchezo wa soka nchini England, FA lingemuadhibu Ferguson kwa kukabiliana na maafisa waliokuwa wakisimamia mechi hiyo ambayo Manchester United ilishinda kwa magoli 4-3, katika uwanja wa Old Trafford.

'' Allan Pardew ndiye kocha ambaye mara nyingi huwazomema marefa kwa takriban karibu mechi zote'' alisema Ferguson.

Pardew alipigwa marufuku ya kutohudhuria mecho mbili baada ya kupatikana na hatia ya kumsukuma mmoja wa wasimamizi wa mechi yao mwezi Agosti.

Ferguson alimzomea refa wa mechi hiyo Mike Dean, naibu wake Jake Collin na Neil Swarbrick, mwanzo wa kipindi cha pili ya mechi yao ya ligi kuu ya Premier kupinga goli la pili la Newcastle.

Dean aliidhinisha kuwa Papiss Cisse, hakuwa ameotea wakati Jonny Evans alipojifunga kunako dakika 28.

Pardew hakufurahiswa na uamuzi wa FA wa kutomuadhibu kocha huyo wa Manchester United mwenye umri wa miaka sabini.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.