Mancini akiri wanakabiliwa na tatizo kubwa

Imebadilishwa: 27 Disemba, 2012 - Saa 14:59 GMT
Roberto Mancini

Roberto Mancini

Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini, amesema klabu hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa kufuatia kushindwa kwa bao moja kwa bila na Sunderland.

Mabingwa hao watetezi, walipoteza nafasi nyingi za kufunga wakati wa mechi hiyo, na kupoteza alama tatu muhimu, hatua inayowaweka alama saba nyumba ya vinara wa sasa Manchester United.

Man City imefunga magoli 34 baada ya kucheza mechi 19, katika mechi za ligi kuu msimu huu, idadi ambayo ni magoli kumi na nne chini ya magoli waliyofunga mahasimu wao Manchester United ambao waliilaza Newcastle 4-3 siku ya Jumatano.

Zaidi ya yote Man City imefunga magoli 12 kwa mechi tisa za ugenini ukilinganisha na United ambayo imefunga magoli 22 kutoka kwa mechi 10.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.