Arsenal yairarua New Castle 7-3

Imebadilishwa: 29 Disemba, 2012 - Saa 20:47 GMT
Walcott akielekea katika lango la Newcastle

Walcott akielekea katika lango la Newcastle, Arsenal ilipoifunga Newcastle mabao 7-3

Arsenal imeiangushia kipigo kikali New Castle kwa kuicharaza magoli 7-3 katika mchezo wa ligi kuu ya England uliofanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Emirates.

Theo Walcott alikuwa mwiba katika ngome ya New Castle baada ya kuibuka na magoli matatu kati ya saba yaliyofungwa na Arsenal, Jumamosi katika mchezo uliofanyika uwanja wa Emirates.

Walcott pia alichangia upatikanaji wa magoli mawili zaidi kwa kutoa pasi nzuri kwa wafungaji.

Kwa matokeo hayo Arsenal imepanda hadi nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu ya England.

Arsenal ilianza kujipatia bao la kwanza katika dakika ya 20 kupitia kwa Theo Walcott, lakini Demba Ba aliisawazishia Newscastle katika dakika ya 43 na hivyo hadi kipindi cha kwanza timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa Arsenal tena kufunga kupitia kwa Oxlade-Chamberlain katika dakika ya 50.

Newcastle wakasawazisha tena kupitia kwa Sylvain Marveaux. Baadaye dakika ya 64 Podolski alifunga goli la tatu kwa Arsenal na Demba Ba akaifisawazishia tena Newcastle na kufanya mchezo kusomeka 3-3.

Baada ya hapo ndipo mvua ya magoli ikaanza kuinyeshea Newcastle kwa Walcott kufunga magoli katika dakika ya 73 na 90, huku Olivier Giroud akiifungia Arsenal katika dakika ya 84 na 87.

Theo Walcott aliondoka na mpira baada ya kufunga magoli matatu.

Matokeo ya michezo mingine ya ligi kuu iliyochezwa Jumamosi:

Sunderland 1-2 Tottenham

Aston Villa 0-3 Wigan

Fulham 1-2 Swansea

Man U 2-0 West Brom

Norwich 3-4 Manchester City

Reading 1- 0 West Ham

Stoke 3- 3 Southampton

Kwa matokeo hayo Machester United inaoongoza kwa pointi 49 katika michezo 20 iliyocheza ikifuatiwa na Manchester City pointi 42, Totenham 36 na Chesea nafasi ya nne pointi 35. Hata hivyo Arsenal na Everton zenye pointi 33 zimecheza michezo 19, huku Chelsea yenye pointi 35 ikiwa imecheza mechi 18.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.