Liverpool yaididimiza QPR 3-0

Imebadilishwa: 30 Disemba, 2012 - Saa 19:02 GMT
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia bao

Wachezaji wa Liverpool wakishangilia bao


Liverpool ambayo mwenendo wake katika ligi kuu ya England umekuwa wa kusuasua, katika mechi yao ya Jumapili kwenye uwanja wa QPR, waliwacharaza wenyeji mabao 3-0.

QPR iliyo mkiani mwa ligi kuu ya England imezidi kupoteza matumaini ya kubakia katika ligi hiyo baada ya kuendelea kupoteza pointi katika michezo yake.


Mshambuliaji machachari wa Liverpool ndiye ayelikuwa mwiba kwa vijana wa Harry Redknapp pale alipoifungia timu yake la Liverpool magoli mawili katika kipindi cha kwanza cha mchezo ikiwa ni katika dakika ya 10 na 16, huku Agger akiihakikishia Liverpool ushindi wa pointi tatu pale alipofyatua bao la tatu katika dakika ya 28 ya mchezo.

Kwa matokeo hayo Liverpool imejisogeza hadi nafasi ya 9 ikiwa na pointi 28 katika mechi 20 ilizocheza, na kuonyesha dhamira ya kurejea katika ubora wao wa zamani kwa kuwa miongoni mwa timu nne za England zinazowania kushiriki michuano mikubwa ya bara la Ulaya.

Kwa idadi hiyo hiyo ya mechi QPR wana pointi 10 tu, hali inayotishia kuendelea kuwepo kwao katika ligi kuu ya England msimu ujao.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.