Demba Ba asajiliwa rasmi na Chelsea

Imebadilishwa: 4 Januari, 2013 - Saa 12:44 GMT

Demba Ba

Chelsea imethibitisha kuwa imemsajili mshambulizi wa Newcastle Demba Ba, kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu.

Inaaminika kuwa Kandarasi ya Demba Ba na Klabu ya Newcastle, ilikuwa na kifungu kinamruhusu kuzungumza na vilabu vingine ikiwa vitakuwa tayari kulipa pauni millioni saba.

Akiongea muda mfupi baada ya kusajiliwa Ba, amesema kuwa ana furaha nyingi kujiunga na klabu hiyo.

Mshambulizi huyo kutoka Senegal ameongeza kusema kuwa ikiwa klabu yoyote ilishinda kombe la klabu bingwa barani ulaya ikitaka kukusajili, mara nyingi uamuzi ni wa haraka.

Ba alijiunga na Newcastle kutoka klabu ya West Ham mwezi Juni mwaka 2011, kuchukua mahala pa Daniel Sturridge ambaye alijiunga na klabu ya Liverpool mapema wiki hii kutoka kwa klabu ya Chelsea.

Kwa mujibu wa sheria mpya Ba, ataichezea Chelsea mechi ya ya kuwania kombe la FA siku ya Jumamosi dhidi ya Southampton na pia mechi ya kuwania kombe la ligi dhidi ya Swansea, lakini hatacheza mechi ya kuwania kombe la Uropa kwa kuwa alikuwa ameichezea klabu ya Newcastle.

Ba, amefunga jumla la magoli 13 msimu huu na usajili wake unatarajiwa kuwa na manufaa makubwa kwa Chelsea kwa kuwa atashirikiana na Fernando Torres ambaye alisajiliwa kwa kitita cha pauni milioni hamsini.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.