Mancini agombana na Balotelli

Imebadilishwa: 3 Januari, 2013 - Saa 17:10 GMT

Mancini akimvuta shati Baloteli

Mshambulizi wa Manchester City Mario Balotelli amezozana na kocha wake Roberto Mancini wakati walipokuwa mazoezini.

Picha za wawili hao wakivutana mashati zimesambazwa kwa vyombo vya habari na inasemekana zilizchukuliwa mapema hii leo wakati walipokuwa mazoezini katika uwanja wa Carrington.

Picha hizo zimeonyesha wachezaji wengine na maafisa wa klabu hiyo wakijaribu kuwatenganisha.

Hata hivyo klabu hiyo imekataa kuthibitisha au kukanusha madai hayo.

Mancini anatarajiwa kujibu maswali kuhusu tukio hilo wakati atakapofanya kikao na waandishi wa habari siku ya Ijumaa.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.