Demba Ba aifungia Chelsea magoli mawili

Imebadilishwa: 6 Januari, 2013 - Saa 12:39 GMT

Demba Ba akisherehekea bao lake

Demba Ba alifunga mabao mawili wakati wa mechi yake ya kwanza na Chelsea ya kuwania kombe la FA dhidi ya Southampton.

Wenyeji Southampton ndio waliokuwa wa kwanza kufunga kupitia kwa nyota wao Jay Rodriguez.

Ba ambaye alisajiliwa na Chelsea siku ya Ijumaa wiki hii, aliifingia Mabingwa hao watetezi wa kombe hilo bao lao la kwanza baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Juan Matta.

Victor Moses naye akafunga goli la pili na kuiweka Chelsea mbele kwa 2-1, kabla ya Branislav Ivanovic kufunga bao la tatu kwa kichwa.

Na kudhihirisha umaarufu wake, kwa mara nyingine Demba Ba alifunga bao la nne baada ya kupewa pasi nyingine maridadi kutoka kwa Eden Hazard.

Masaibu ya Southampton hayakuishia hapo, na Chelsea ilipata bao lingine kupitia kwa naodha wake Frank Lampard, ambaye alifunga kupitia kwaju wa penalti kunako dakika ya themanini na tatu.

Lampard sasa anashikilia nafasi ya pili miongoni mwa wachezaji walioifungia Chelsea magoli mengi zaidi.

Lampard ameifungia Chelsea magoli 193 sawa na Kerry Dixon.

Kutokana na mechi ya jana, Chelsea iliimarisha nafasi yake ya kuhifadhi kombe hilo ambalo ilishinda katika fainali ya msimu uliopita dhidi ya Liverpool kwa magoli 2-1.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.