Droo ya raundi ya nne ya kombe la FA

Imebadilishwa: 6 Januari, 2013 - Saa 15:55 GMT

Chelsea ikisherehekea ushindi wa kombe la FA mwaka wa 2012

Droo ya raundi ya nne ya michuano ya FA imetangazwa.

Mabingwa watetezi wa kombe hilo Chelsea imepangiwa kucheza na mshindi wa mechi kati ya Southend United na Brentford.

Mshindi wa mechi kati ya West Ham United na Manchester United atachuana na mshindi wa mechi kati ya West Fulham na Blackpool.

Mabingwa wa wa ligi kuu ya Premier Manchester City nayo imeratibiwa kucheza na mshindi wa mechi kati ya
Crystal Palace na Stoke City.

Baada ya kutoka sare ya kufungana magoli mawili kwa mawili hii leo mshindi wa raindi ya pili kati ya Swansea na Arsenal atapambana na mshindi wa mechi kati ya Brighton na Hove Albion.

Mechi zingine Huddersfield Town itatoa udhia dhidi ya Leicester, mshindi wa mechi kati ya QPR na West Brom atacheza na mshindi wa mechi nyingine ya marudio kati ya Sheffield Wednesday na MK Dons.

Mshindi wa mechi kati ya Bolton na Sunderland atapepetana na mshindi wa mechi kati ya Cheltenham na Everton

Ratiba ya mechi zingine za raundi ya nne

Hull City au Leyton Orient vs Barnsley

Middlesbrough vs Aldershot Town

Millwall v Aston Villa

Leeds United au Birmingham City vs Tottenham Hotspur

Norwich City vs Luton Town

Oldham Athletic vs Mansfield Town au Liverpool

Macclesfield Town vs Wigan Athletic au Bournemouth

Derby County vs Blackburn Rovers

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.