Sergio Aguero yuko italia kwa matibabu

Imebadilishwa: 6 Januari, 2013 - Saa 13:18 GMT

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya premier, Manchester City, walizika tofauti zao na kujikatia tikiti ya raundi ijayo ya kombe hilo la FA.

Manchester City, iliilaza Watford kwa magoli matatu kwa yai.

Timu hiyo ilikuwa imeangaziwa pakubwa na vyombo vya habari kutuatia mzozo kati ya kocha na Roberto Mancini na Mario Balotelli.

Carlos Tevez na Gareth Barry walifunga bao moja kila mmoja katika kipindi cha kwanza kabla ya Marcos Lopes kuongeza la tatu.

Balotelli, ambaye alizozana na kocha huyo alicheza kipindi cha pili kama mchezaji wa ziada.

Wakati huo huo mshambulizi wa Manchester City Sergio Aguero, amethibitisha kuwa alipata jeraha la paja na kwa sasa yuko nchini Italia kupata matibabu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, kutoka Argentina, alipata jeraha hilo wakati wa mechi yao dhidi ya Stoke City Tarehe moja mwezi huu, na hakucheza mechi yao dhidi ya Watford.

Haijulikani ni lini mchezaji huyo atarejea tena lakini wasimamizi wa Manchester City, wanasema huenda akashirikishwa katika mechi yao dhidi ya Arsenal wikendi ijayo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.