Tevez aapa kufuata nyayo za Van Persie

Imebadilishwa: 10 Januari, 2013 - Saa 13:28 GMT

Carlos Tevez

Mshambulizi wa Manchester City, Carlos Tevez, amesema kuwa washambulizi wa klabu hiyo wamepata motisha zaidi, baada ya kocha wao kumsifu mshambulizi wa Manchester United Robin Van Persie.

Hivi majuzi, Mancini, alikiri kuwa anajuta kwa nini klabu hiyo haikumsajili Van Persie, ambaye kufikia sasa amefunga magoli 20 msimu huu.

Mancini alisema kuwa tofauti kati ya timu hizo mbili ni mchezaji huyo.

Manchester City inashikilia nafasi ya pili, alama saba nyuma ya mahasimu wao Manchester United, huku mechi kumi na saba zikiwa zimesalia.

United iliilaza City magoli 3-2 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Etihad tarehe 9 Decemba mwaka uliopita.

Timu hizo mbili zimepangiwa kuchuana tena tarehe 6 April katika uwanja wa Old Trafford na Tevez anasema wao na kibarua kigumu kuwapiku mahasimu hao wa jadi, lakini watapambana kadri ya uwezo wao kushinda mechi zinazofuata kabla ya mechi hiyo ngumu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.