Chelsea yailaza Stoke 4-0

Imebadilishwa: 12 Januari, 2013 - Saa 18:04 GMT

Frank Lampard akisherehekea bao lake

Jon Walters alifunga magoli mawili katika lango na kupoteza mkwaju wa penalti huku Chelsea ikiilaza Timu yake ya Stoke City kwa magoli 4-0.

Kufuatia ushindi huo Chelsea sasa imevunja rekodi ya Stoke City ya kutoshindwa katika mechi yoyote katika uwanja wao wa nyumbani.

Kabla ya mechi hiyo Stoke ilikuwa imecheza mechi 17 katika uwanja wao bila kupoteza hata moja.

Walters aliifungia Chelsea bao la kwanza kwa kichwa baada ya Cesar Azpilicueta kupiga cross, na wakati alipokuwa akijaribu kuiondoa, kwa bahati mbaya likaingia ndani ya lango lao.

Dakika ya 45 kipindi cha kwanza Walters alifanya kosa kama hilo hilo na kufunga kwa mara nyingine kwa kichwa cross iliyopigwa na Juan Mata corner.

Frank Lampard naye akaifungia Chelsea bao la tatu kupitia kwa mkwaju wa penalti kabla ya Eden Hazard kufunga la nne kwa kombora alioupiga kwa zaidi ya mita 30 kutoka kwa goli.

Na kipindi hicho cha pili Stoke walipata penalti baada ya John Terry kumfanyia madhambi mchezaji wake lakini mkwaju wa
Walters uligonga mlingoti.

Matokeo mengine ya mechi za ligi kuu.

QPR 0 - 0 Tottenham

Aston Villa 0 - 1 Southampton

Everton 0 - 0 Swansea

Fulham 1 - 1 Wigan

Norwich 0 - 0 Newcastle

Reading 3 - 2 West Brom

Stoke 0 - 4 Chelsea

Sunderland 3 - 0 West Ham

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.