Tevez kusaini mkataba mpya-Mancini

Imebadilishwa: 12 Januari, 2013 - Saa 18:13 GMT

Carlos Tevez

Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini, asema anatarajia kuwa mazungumzo kuhusu kandarasi ya nyota wake Carloz Tevez yataanza hivi karibuni.

Tevez, mwenyi umri wa miaka 28, alijiunga na Manchester City mwaka wa 2009 na nusura mchezaji huyo akihame klabu hiyo pale Mancini aliposhutumu kwa kutokubali kuingia uwanjani kama mchezaji wa ziada, kabla ya kurejea nyumbani kwao Argentina.

Hata hivyo mzozo huo ulitatuliwa na Tevez alirejea tena na kuisadia Manchester City, Kushinda kombe la ligi kuu ya Premier mwaka uliopita, kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1968.,

Mkataba wake na klabu hiyo inatarajiwa kukamilika mwaka wa 2014 na Mancini amesema ana matarajio makubwa kuwa mchezaji huyo kutoka Argentina atasaini kandarasi mpya.

Kwingineko, Liverpool, imesitisha kandarasi ya mchezaji wake Nuri Sahin, ambaye alikuwa akiicheza kwa mkopo.

Sahin sasa ataichezea klabu ya Borussia Dortsmund kwa muda wa miezi kumi na nane ijayo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alijoiunga na Liverpool, Agosti mwaka uliopita, kutoka klabu ya Real Madrid na alitarajiwa kuicheza Liverpool msimu huu.

Lakini baada ya kuichezea mechi kumi na mbili pekee na kufunga magoli matatu pekee, kocha wa Liverpool, Brendan Roggers ameamua kusitisha kandarasi ya mchezaji huyo.

Mchezaji huyo kutoka Uturuki, alianza kucheza soka ya kulipwa na klabu ya Dortmund na mwaka wa 2011, aliisaidia klabu hiyo kushinda ligi kuu ya Ujerumani na pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka, mwaka wa 2010.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.