Arsenal yaadhibiwa nyumbani 2-0 na Man City

Imebadilishwa: 13 Januari, 2013 - Saa 18:53 GMT

Wachezaji wa Manchester United wakishangilia bao lao

Manchester City imeilaza Arsenal magoli 2-0 katika mechi iliyojawa na msisimuko iliyochezwa katika uwanja wa Emirates na kudumisha matumaini yao ya kuhifadhi kombe hilo kwa mwaka wa pili mfululizo.

Mcheza kiungo cha wa Arsenal Laurent Koscielny alipewa kadi nyekundu kunako dakika ya 10, baada ya kumfanyia madhambi Edin Dzeko, lakini mkwaju wa Dzeko uliokolewa na kipa wa Arsenal.

Hata hivyo dakika chache baadaye James Milner aliifungia mabingwa hao watetezi bao lao la kwanza kabla ya Dzeko kufidia penalti aliyopoteza kwa kufunga bao la pili.

Katika kipindi hicho cha pili, Arsenal ilionekana kujiimarisha laki ni juhudi zao hazikufua dafu.

Sawia na ilivyokuwa katika kipindi cha kwanza naodha wa Manchester City Vincent Kompany alipewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Jack Wilshere.

Manchester City bado ingali katika nafasi ya pili na alama 48 alama saba nyuma ya vinara wa ligi hiyo kwa sasa Manchester United.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.