Kocha wa DRC hajajiuzulu asema Waziri

Imebadilishwa: 18 Januari, 2013 - Saa 16:50 GMT

Kocha wa Congo Claude Le Roy

Huku ikiwa imesalia chini ya saa ishini na nne kabla ya kuanza kwa fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini, timu ya taifa ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imekubwa na mzozo.

Ripoti zinasema kocha mkuu Congo Claude Le Roy,ametangaza nia yake ya kujiuzulu.

Le Roy mwenye umri wa miaka 64 raia wa Ufaransa, amekasirishwa na maandalizi duni ya timu hiyo.

awali kulikuwa na ripoti kuwa amewasilisha barua ya kujiuzulu afisa wa Shirikisho la soka DRC.

Lakini akiongea na waandishi wa habari kocha huyo amesema hana uhakika ikiwa ataendelea kuwa mkufunzi wa timu hiyo.

Lakini rais wa shirikisho la mchezo wa soka nchini DRC, amepuuzilia mbali madai kuwa kocha huyo amejiuzulu.

Kashfa hii sio geni kwa DRC

Timu ya taifa ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Omari Selemani amekanusha madai kuwa kocha huyo amejiuzulu kuhusiana na kashfa ya malipo ya ziada kwa wachezaji wake.

'' Claude bado ni kocha wetu na ataongoza kikosi chetu dhidi ya Ghana'' Alisema Selemani.

DR Congo inacheza mechi yao ya ufunguzi ya kundi B dhidi ya Black Stars YA Ghana, mjini Port Elizabeth siku ya Jumapili.

Kashfa ya malipo ya ziada kwa wachezaji wa Congo sio jambo geni kwa wachezaji hao na kocha huyo.

Wakati wa michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika mwaka wa 2006, wachezaji wa DRC walitishia kutocheza mechi yao na Togo, hadi pale rais Joseph Kabila, alipowahaidi kulipa malipo yao ya ziada muda mfupi kabla ya mechi yao.

Mzozo huo uliadhiri matayarisho ya kocha huyo na tukio hilo limetokea kwa mara nyingine tena.

Waziri akiri kocha ana sababu ya kutaka kujiuzulu

Afisa anayehusika na masuala ya habari wa Congo, amekiri kuwa kumekuwa na uhasama mkali kati ya kocha huyo na viongozi wa shirikisho la mchezo wa soka kuhusiana na malipo ya wachezaji.

Wachezaji wa Ghana watakaocheza na DRC

Kocha huyo kutoka Ufaransa, ambaye aliongoza Cameroon kushinda kombe hilo mwaka wa Themanini na nane, amepata sifa kubwa nchini Congo kwa kuiwezesha timu hiyo kufuzu kwa fainali hizo kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka saba iliyopita.

Waziri wa michezo wa Congo Banza Mukalay vile vile amekanusha kujiuzulu kwa kocha huyo na kusema kukiri kuwa malipo ya wachezaji yalikuwa yamechelewesha sana.

Waziri huyo amesema tatizo hilo limesababisha na kuongezeka kwa maafisa wanaoambatana na timu hiyo ambao pia wanataka malipo ya ziada.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.