Ghana kupepetana na DRC

Imebadilishwa: 19 Januari, 2013 - Saa 21:22 GMT

Wachezaji wa Ghana

Timu za Ghana na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kesho zinajitupa katika mchezo wa ufunguzi wa kundi B nchini Afrika Kusini. Mali na Niger zitapambana katika mechi ya pili ya kundi hilo.

Ghana na Mali zinapewa nafasi ya kuibuka washindi wa kwanza katika kundi hilo kutokana na ubora wa vikosi hivyo katika miaka michache iliyopita.

Hata hivyo wakati wa mechi za kufuzu, DR.Congo maarufu kama Leopards kuicharaza Seychelles jumla ya magoli 7-0 katika mzunguko wa kwanza na kufuatiwa na ushindi wa jumla ya 5-2 dhidi ya Equatorial Guinea - ina maana DR Congo si timu ya kupuuza.

DRC ina kocha Claude Le Roy, ambaye ana uzoefu katika kandanda barani Afrika. Kocha huyo Mfaransa imeweza kuziongoza timu katika fainali hizo mara saba.

Je, DRC itajiongezea mataji yake baada ya yale ya mwaka 1968 na 1974? Hilo ni suala la kusubiri na kuona.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.