Man City yaikaribia Man United

Imebadilishwa: 19 Januari, 2013 - Saa 19:02 GMT

David Silva

David Silva alifunga magoli mawili na kuisadia Manchester City, kuilaza Fulham katika uwanja wao wa Etihad na kupunguza idadi ya alama kati yao na vinara wa sasa Manchester United.

Kufuatia ushindi huo, wa magoli mawili kwa bila mabingwa hao watetezi wako alama nne nyuma Manchester United.

United hata hivvyo inaweza kurejesha uongozi wao wa alama saba hapo kesho ikiwa watashinda mechi yao dhidi ya Tottenham.

Katika mechi nyingine, kwa mara ya kwanza washambulizi wa Liverpool Luis Suarez na Daniel Sturridge walicheza pamoja katika mechi moja na kila mmoja wao kufunga bao wakati wa mechi yao dhidi ya Norwich.

Liverpool ilishinda mechi hiyo kwa kuinyuka Norwich magoli matano kwa yai.

Luis Suarez

Newcastle nayo ilipoteza alama tatu muhimu katika uwanja wao wa nyumabani pale ilipolimwa magoli mawili kwa moja na Reading.

Adam Le Fondre ambaye aliingia kama mchezaji wa ziada alifunga magoli mawili katika muda wa dakika sita.
Kufuaia kipigo hicho, Newcastle sasa imeshuka hadi nafasi ya 17 na alama 21.

Newcastle hata hivy7o ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufunga kupitia kwa mshambulizi wake Yohan Cabaye.

Jonathan de Guzman alifunga magoli mawili naye Ben Davies akafunga bao moja na kuhakikishia Swansea, alama tatu muhimu za ligi kuu ya premier.

Swansea iliinyeshea Stoke City magoli matatu kwa moja.

Katika matokea mengine West Ham ilitoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na QPR nayo Wigan ikafunga magoli 2 - 3 na Sunderland.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.