Manchester United yavutwa shati.

Imebadilishwa: 20 Januari, 2013 - Saa 18:58 GMT

Mshambuliaji wa Van Persie akishangilia goli

Vinara wa ligi kuu ya England, Manchester United imeambulia pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Tottenham.

Mshambuliaji Robin Van Persie aliiwezesha timu yake ya Manchester United kuongoza kipindi cha kwanza baada ya kufunga bao katika dakika ya 25.

Van Persie alipata goli hilo akiunganisha krosi ya Tom Cleverly.

Man United wakiamini kuwa tayari wamepata ushindi katika mechi hiyo, walijikuta wakigawa pointi baada ya Clint Dempsey kufunga katika dakika za majeruhi na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa Tottenham katika uwanja wao wa White Hart Lane.

Matokeo hayo bado yanaiacha Manchester United kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 56, huku ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 51.

Tottenham iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 41, pointi nne nyuma ya Chelsea yenye pointi 45, ikikakalia nafasi ya tatu ya ligi kuu ya England.

Timu zote hizo nne zimecheza mechi 23 kila moja.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.