Chelsea yailaza Arsenal 2-1

Imebadilishwa: 20 Januari, 2013 - Saa 15:41 GMT

Frank Lampard

Chelsea imeweza kupata pointi tatu muhimu katika kinyang'anyiro cha ligi kuu ya England baada ya kuilaza Arsenal magoli 2-1 katika uwanja wa Stanford Bridge.

Juan Mata alipachika bao la kwanza la Chelsea kabla ya Frank Lampard kufunga bao la pili kupitia mkwaju wa penalti.

Hata hivyo Arsenal kupitia kwa mshambuliaji wake Theo Walcott aliweza kufunga bao zuri, akiwazidi maarifa walinzi wa Chelsea pamoja na mlinda mlango wao.

Kipindi cha Arsenal ilizidi kuibana Chelsea ambapo ilipata kona tisa dhidi ya tatu za Chelsea. Hata hivyo mechi hiyo ilimalizika kwa Chelsea kuibuka na ushindi huo wa magoli mawili kwa moja.

Huu ni ushindi wa kwanza kwa Chelsea katika uwanja wake mwaka huu 2013 kati ya mechi nne ilizocheza uwanjani hapo Stanford Bridge.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.