Sir Alex Ferguson amkashifu refa

Imebadilishwa: 21 Januari, 2013 - Saa 14:59 GMT

Sir Alex Ferguson

Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson, ameshutumu msaidizi wa refa Simon Beck kwa kumyima Wayne Rooney penalti ya wazi wakati wa mechi yao na Tottenham Hotspurs, ambayo timu hizo mbili zilitoshana nguvu ya kufungana bao moja kwa moja katika uwanjawa White Hart Lane.

Ferguson ameshutumu msaidizi huyo wa refa, hasa baada ya Clint Dempsey kufunga bao kunako dakika ya mwisho ya mechi hiyo na kuinyima United alama tatu muhimu na kupunguza uongozi wao kutoka alama saba hadi tano mbele ya mabingwa watetezi Manchester City.

Ferguson alisema'' miaka kadhaa iliyopita msaidizi huyo wa refa, alimuachilia mshambulizi wa Chelsea Didier Drogba ambaye alikuwa tayari ameotea kufunga bao''.

Kocha huyo amesisitiza kuwa walimyinwa penalti halali na kuwa mechi hiyo ilisimamia vibaya sana.

Van Persie na Wayne Rooney

Hii sio mara ya kwanza kwa Fergusoj kutofautiana na refa huyo.

Mwaka wa 2010 kocha huyo wa Manchester United alikasirishwa sana na uamuzi wa kumruhusu Didier Drogba kufunga licha ya kujenga kibanda katika eneo lao.

Wakati wa mechi hiyo Chelsea iliishinda Manchester United katika uwanja wao wa nyumbani na kivyo kuimarisha matumaini yao ya kunyakuwa kombe la ligi kuu msimu huo.

Lakini katika mechi ya siku ya Jumapili, Wayne Rooney aliangushwa na mlinda lango wa Spurs Steven Caulkerkatika kipindi cha pili lakini refa hakutoa adhabu yoyote.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, mshambulizi wa Manchester United, Wayne Rooney alidai kuwa Caulker alimuangusha, lakini hakutaka kubishana naye ili kuhujumu kile alichokitaja kama juhudi zao wakati wa mechi hiyo.

Koch a wa Spurs Andre Villas-Boas kwa upande wake amesema hana uhakika ikiwa Caulker, alimfanyia Rooney madhabmbi.

Kocha huyo amesema mbali na tukio hilo, anahisi kuwa maamuzi mengi wakati wa mechi hiyo yalikwenda kinyume na matarajio yao na kuwa walipoteza nafasi nyingi za kufunga.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.