Nigeria yatoka sare ba Burkina Faso 1-1

Imebadilishwa: 21 Januari, 2013 - Saa 20:13 GMT

Wachezaji wa Nigeria wakisherekea bao lao

Nigeria imeanza kampeini yake ya kinyang'anyiro cha kuwania kombe la Mataifa ya Afrika, nchini Afrika Kusini kwa kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na Burkina Faso katika mechi yao ya ufunguzi ya kundi C.

Nigeria ilipata bao hilo muhimu na la ushindi kupitia kwa msahmbulizi wake Emmanuel Emenike, anayeichezea klabu ya Spartak Moscow ya Urussi kunako dakika ya 23.

Kikosi hicho cha Super Eagles, kilifanya mashambulizi kadhaa katika lango la Burkina Faso, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda.

Baada ya dakika za kwanza 45, zilimalizika huku Nigeria ikiwa kifua mbele kwa bao moja kwa bila.

Awali Nahodha wa Nigeria Joseph Yobo alisema kushinda kombe hilo sio kazi rahisi, ila wamejitolea kucheza kadri ya uwezo wao, kuhakikisha kuwa Nigeria, inaibuka mshindi.

Wachezaji wa Burkina Faso wakisherehekea bao lao

Amesema dhamira yao kuu, ni kufikiria hatua za robo na nusu fainali.

Mcheza kiungo, Victor Moses ambaye anaiakilisha Nigeria kwa mara ya kwanza naye anasema wamejianda vyema na ana matarajio makubwa kuwa watafanya vyema katika mashindano ya mwaka huu.

Matumaini ya kocha wa Super Eagles, Stephen Keshi, ambaye anaiongoza timu kwa mara ya kwanza katika fainali hizo ya kuandikisha ushindi wake wa kwanza ulitumbukia nyongo pale Burkina Faso iliposawazisha katika dakika za ziada.

Timu zote katika kundi hilo, Ethiopia, Burkina Faso, Nigeria na Zambia sasa zina alama moja kila mmoja.

Nigeria sasa itachuana na Zambia katika mechi yao ijayo kisha icheza na Ethiopia mechi yao ya mwisho ya makundi.

Burkina Faso nayo imeratibiwa kucheza na Ethiopia mechi ijayo kisha ikamilishe kampeinin yake ya raundi ya kwanza na Zambia.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.