Morocco 0 Cape Verde 0

Imebadilishwa: 23 Januari, 2013 - Saa 17:57 GMT

Wachezaji wa Cape Verde kabla ya mechi hiyo

Mabingwa za zamani wa kombe la mataifa ya Afrika, Morocco, kwa mara nyingine wamerejea uwanjani kumenyana na Cape verde katika mechi yao ya pili ya mashindano hayo yanayoendelea nchini Afrika Kusini.

Morocco inaanza mechi hiyo ikiwa na matumaini makubwa ya kuimarisha nafasi yake ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo, kwa kunadikisha ushindi wao kwa kwanza.

Lakini ombi hilo litatimia ikiwa wachezaji wa Morocco wataimarisha safu yao ya mashambulizi, kwa kuwa katika mechi yao ya ufunguzi, walipigwa mikwaju mitatu pekee iliyolenga goli wakati wa mechi yao na Angola.

Nyota wa Morocco Younes Belhanda, anayeichezea klabu ya Montepilier huenda akacheza mechi ya leo ili kuimarisha safu hiyo ya mashambulizi.

Kwa upande mwingine Cape Verde huenda ikakosa huduma za wachezaji wake nyota Toni Varela na Babanco, ambao walikuwa wakiuguza majereha.

Cape Verde yapania kushinda mechi yake ya kwanza

Younes Belhanda

Lakini licha ya wasi wasi hizo, kocha wa Cape verde Luis Antunes, ana matumaini makubwa kuwa kikosi chake ambacho kinashiriki katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza wanaweza kuandikisha ushindi wao wa kwanza.

Cape Verde, sawa na Morocco, ilitoka sare ya kutofungana bao lolote katika mechi yao ya ufunguzi, lakini ilionyesha mchezo mzuri kuliko wapinzani wao Afrika Kusini.

'' Tulikuwa na nafasi nyingi za kufunga katika mechi yetu ya kwanza lakini hatukuzitumia'' Alisema kocha wa Morocco baada ya mechi yao ya kwanza dhidi ya Angola.
Rachid Taoussi, Morocco coach:

''Naamini kuwa tunaweza kufanya vyema kuliko tulivyocheza wakati wa mechi yetu na Cape Verde na Afrika Kusini siku ya Jumapili'' Aliongeza kocha huyo.

Lakini kocha wa Cape Verde anasema matokeo yao dhidi ya Afrika Kusini ambao ni wenyeji wa mashindano hayo, yamewapa matumaini makubwa.

Anasema kabla ya mashindano hayo, hakuna aliyedhania kuwa wawo watapata hata alama moja wakati wa fainali hizo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.