Je De Gea ni kipa bora zaidi?

Imebadilishwa: 23 Januari, 2013 - Saa 12:54 GMT

David de Gea

Aliyekuwa kuwa kipa nambari moja wa Manchester United Roy Carroll, amesema anaamini kuwa kocha wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson, atamdumisha David de Gea kama kipa nambari moja wa klabu hiyo.

Ripoti zinasema kuwa kipa huyo kutoka uhispania huenda akauzwa baada ya kufanya makosa mengi tangu alipojiunga na Manchester United kutoka kwa klabu ya Atletico Madrid, mwaka wa 2011 kwa kitita cha pauni milioni kumi na nane.

Akiongea na BBC Carol amesema, anasikitika sana kuhusu hali ya kipa huyo kwa sasa.

''Wakati unapofanya makosa watu hawawezi kusahau kwa haraka na kama kipa mchanga ni jambo gumu sana'' Alisema Carol.

Carol aliongeza kuwa De Gea kwa sasa anahitaji kuungwa mkono na kocha wake, kwa sababu, tangu aliposajiliwa, amecheza mechi nyingi.

Caroll, anayeichezea klabu ya Olimpiakos ya Ugiriki anasema De Gea bado ni miongoni mwa makipa bora zaidi duniani na pia bado angali mchanga.

''Kumekuwa na mabadiliko mengi katika safu ya ulinzi ya Manchester United msimu huu, kutokana na majeraha, kwa hivyo nahisi huu ni wakati mgumu sana kwa kipa huyo''

Caroll, ambaye alijiunga na Manchester United kutoka kwa klabu ya Wigan mwaka wa 2011 amekiri kufanya makosa mengi wakati alipokuwa akiichezea kwa miaka minne.

De Gea alishutumiwa hivi majuzi kufuatia uamuzi wake wa kukosa kuutema mpira nje na hivyo kuipa Tottenham nafasi ya kusawazisha na kuinyima United alama tatu muhimu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.