Afrika Kusini imeilaza Angola 2-0

Imebadilishwa: 23 Januari, 2013 - Saa 17:10 GMT

Wachezaji wa Afrika Kusini

Afrika Kusini imefufua matumaini yake ya kufuzu kwa raundi ijayo ya michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Afrika Kusini, kwa kuilaza Angola kwa magoli mawili kwa bila, katika mechi yaon ya pili siku ya Jumatano.

Vijana hao wa Bafana Bafana walianza mechi hiyo vyema kuliko walivyocheza katika mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Cape Verde.

Katika kipindi cha kwanza ilifanya mashambulizi kadhaa katika lango la Angola.

Kunako dakika ya kumi na tano Afrika nusura ifunge bao lakini msaidizi wa refa wa mechi hiyo aliinua kijibendera kuashiria kuwa alikuwa ameotea.

Dakika mbili baadaye Bafana Bafana ilifanya shambulio lingine na mkwaju wa Siyabonga Sangwen ulikosa gola kwa ncha.

Wachezaji wa Afrika Kusini wakisherehekea bao lao

Kunako dakika ya 30 Siyabonga Sangweni akaifungia Afrika Kusini bao lake la kwanza.

Bao hilo lilionekana uwapa nguvu wachezaji wa Afrika Kusini ambao waliendeleza mashambulio yao dhidi ya Angola.

Malalamiko ya kocha

Afrika Kusini ingelifunga magoli zaidi katika kipindi hicho lakini wachezaji wake kadhaa walikosa umakini wakati wa kumalizia kwa kupoteza pasi nzuri walizopewa na wakati mwingine kupiga mpira ovyo.

Hata hivyo juhudi zao hazikufanikiwa na kufikia wakati wa mapunziko Afrika Kusini ilikuwa ikiongoza kwa bao moja kwa bila.

Kabla ya mechi hiyo kocha wa Afrika Kusini alikuwa amewashutumu wachezaji wake kwa kukosi umakini wakati wa mechi muhimu na inaonekana kuwa mazungumzo yake na wachezaji wake imeonekana kuzaa matunda.

Kipindi cha pili kilianza huku Angola ikiwa na wachezaji kumi pekee baada ya refa wa mechi hiyo kuanza mpira kabla ya kuruhusu mabadiliko katika kikosi cha Angola.

Kinyume na iliyokuwa katika kipindi cha kwanza wachezaji wa Angola walianza kuonana na kufanya mashambulio kadhaa katika lango la Afrika Kusini.

Lakini, licha ya juhudi hizo, Afrika Kusini ilipata bao lake la pili kunako dakika ya 61 kupitia kwa mchezaji wake wa ziada Lehlohonolo Majoro, ambaye alikuwa ameingia uwanjani dakika mbili tu kabla ya kufunga bao hilo.

Mshambulizi matata wa Angola, Manucho ambaye alitarjiwa kukiongoza kikosi chake kushinda mechi hiyo, alithibitiwa na zaidi ya wachezaji wawili wa Afrika Kusini, mara tu alipopewa pasi.

Angola sasa ni sharti ishinde mechi yake ya mwisho dhidi ya Cape Verde siku ya Jumapili na iombe Morocco itoke sare na Cape Verde katika mechi yao ya Jumatano ili iweze kufuzu kwa hatua ya robo fainali.

Hata hivyo huenda maombi hayo yasitimie ikiwa kutakuwa na mshindi wa mechi ya leo na hivyo Angola italazimika kusubiri matokeo ya mechi kati ya Afrika Kusini na Morocco siku ya Jumapili ili kufahamu ikiwa imeyaaga mashindano hayo au la

Kikosi cha Angola

Kikosi cha Afrika Kusini

01 Lama

03 Lunguinha

04 Massunguna

13 Bastos

15 Miguel

06 Dede

16 Pirolito

18 Da Costa

09 Manucho

17 Mateus

23 Afonso

Wachezaji wa Ziada

12 Landu

22 Neblu

02 Airosa

05 Fabricio

10 Zuela

14 Costa

20 Mingo Bile

07 Djalma

08 Dinis

11 Gilberto

16 Khune

03 Masilela

05 Ngcongca

13 Khumalo

21 Sangweni

15 Furman

18 Thuso Phala

19 Mahlangu

09 Mphela

17 Parker

23 Rantie

Wachezaji wa Ziada

01 Sandilands

22 Meyiwa

02 Gaxa

04 Nthethe

11 Matlaba

08 Tshabalala

10 Serero

12 Letsholonyane

20 Manyisa

07 Majoro

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.