Morocco yatoka sare ya 1-1 na Cape Verde

Imebadilishwa: 23 Januari, 2013 - Saa 18:48 GMT

Wachezaji wa Cape Verde kabla ya mechi hiyo

Cape Verde imeandikisha historia kwa kufunga bao lake la kwanza katika fainali za mataifa ya Afrika yanayoendelea nchini Afrika Kusini.

Cape Verde, amabyo inashiriki katika fainali hizo kwa mara ya kwanza imetoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na mabingwa za zamani wa kombe hilo Morocco, katika mechi ya nne ya kundi A.

Cape Verde, ilipata bao lake kunako dakika ya 36 kupitia kwa nyota wake Platini, ambaye alipokea pasi nzuri kutoka kwa mshambulizi Ryan Mendes

Morocco, ilianza mechi hiyo ikiwa na matumaini makubwa ya kuimarisha nafasi yake ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo, kwa kunadikisha ushindi wao kwa kwanza.

Nyota wa Morocco, Younes Belhanda, wa klabu ya Montepilier ni miongoni mwa wachezea wa Tunisia katika mechi hiyo.

Belhanda alijumuishwa katika kikosi hicho ili kuimarisha safu ya mashambulizi baadaya wa Morocco kutoka sare mechi yake ya ufunguzi.

Cape Verde yapania kushinda mechi yake ya kwanza

Younes Belhanda

Ila tangu kipenga cha mwanzo, Cape Verde ilionekana kuilemea miamba hao wa Afrika Kaskazini.

Kocha wa Cape verde Luis Antunes, ana matumaini makubwa kuwa kikosi chake ambacho kinashiriki katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza watashinda mechi hiyo.

Juhudi za Morocco kusawazisha katika kipindi cha kwanza hazikufua dafu.

Dakika za kwanza arubaini na tano zimekamilika na Cape Verde iko kifua mbele kwa bao moja kwa bila.

Lakini kunako dakika ya sabini na nane Morocco ilizawazisha na kufanya mambo kuwa moja kwa moja.

Cape Verde, sawa na Morocco, ilitoka sare ya kutofungana bao lolote katika mechi yao ya ufunguzi, lakini ilionyesha mchezo mzuri kuliko wapinzani wao Afrika Kusini.

Afrika Kusini inaongoza kundi hilo la alama nne na inahitaji kutoka sare mechi yake ya mwisho ya makundi ili kufuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.

Cape Verde na Morocco zinashikilia nafasi ya pili na alama mbili kila mmoja huku Angolo ikivuta mkia.

Timu hizo tatu sasa ni sharti zishinde mechi zao za mwisho ili kufuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.

Siku ya Alhamisi Mali inacheza na Ghana kisha Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoa udhia Niger katika mechi za kundi B.

Kikosi cha Morocco Kikosi cha Cape Verde

01 Lamyaghri

02 Chakir

03 Bergdich

05 Benatia

17 El Adoua

07 Barrada

08 El Ahmadi

10 Belhanda

11 Assaidi

14 El Hamdaoui

21 Amrabat

Wachezaji wa ziada

01 Lamyaghri

02 Chakir

03 Bergdich

05 Benatia

17 El Adoua

07 Barrada

08 El Ahmadi

10 Belhanda

11 Assaidi

14 El Hamdaoui

21 Amrabat

01 Vozinha

03 Varela

06 Neves

08 Varela

14 Gege

18 Nivaldo

05 Babanco

07 Platini

15 Soares

11 Tavares

20 Ryan

Wachezaji wa Ziada

12 Fock

16 Rilly

13 Lima

19 Pecks

23 Carlitos

02 Stenio

04 Ramos

17 Souto

22 Silva

09 Rambe

10 Heldon

21 Djaniny

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.