Ghana 1 Mali 0

Imebadilishwa: 24 Januari, 2013 - Saa 17:19 GMT

Wachezaji wa Ghana

Timu ya Ghana imeilaza Mali bao moja kwa bila katika mechi yao ya pili ya Kundi B.

Ghana ilipata bao hilo muhimu na la ushindi kupitia mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wake Mubarak Wakaso kuangusha kwenye eneo la hatari.

Goli hilo limefungwa na Wakaso na hivyo kuimarisha nafasi ya Ghana kusonga mbele.

Hadi mapumziko matokeo yalibaki goli 1-0. Kwa matokeo hayo Ghana sasa ina pointi nne, ikifuatiwa na Mali yenye pointi tatu, huku DRC ikiwa na pointi 1 na Niger 0

Kabla ya mechi hiyo Ghana ilifanya mabadiliko matatu katika kikosi chake, Mohammed Rabiu, Isaac Vorsah na Harrison Afful walijumuishwa katika kikosi cha wachezaji wa kwanza kumi na mmoja kuchukua mahali pa Christian Atsu, Derek Boateng na Jerry Akiminko.

Samba Diakite

Kwa upande wake kocha wa Mali pia alifanya mabadiliko kadhaa ambapo, Cheick Fantamady Diarra, Kalilou Traore na Molla Wague waliachwa nje wakati wa mechi yao ya kwanza akianza mechi ya leo.

Momo Sissoko, Adama Coulibaly na Samba Diakite ambao walianza mechi ya ufunguzi kama wachezaji wa ziada, ndio walioanza mechi hiyo ambayo ni sharti washinde ili wafufue matumaini yao ya kufuzu kwa hatua ya robo fainali.


Katika mechi ya kwanza Ghana ilitoka sare ya kufungana magoli 2-2 na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Kikosi cha Ghana Kikosi cha Mali

16 Dauda

04 Pantsil

15 Vorsah

21 Boye

23 Afful

08 Agyemang

10 Adomah

11 Rabiu

20 Asamoah

22 Wakaso

03 Gyan

Wachezaji wa Ziada
01 Adjei
12 Larsen
02 R Boateng
05 Awal
13 Akaminko
19 Mensah
06 Annan
07 Atsu
09 D Boateng
14 Asante
17 Clottey
18 Boakye

01 Samassa
02 Diawara
03 Tamboura
04 A Coulibaly
21 Ndiaye
06 Sissoko
11 S Diarra
12 Keita
17 Abdrahamane Traore
20 Sa Diakite
09 Diabate

Wachezaji wa ziada

16 So Diakite
22 Yirango
05 I Coulibaly
13 Wague
19 S Coulibaly
08 Traore
14 Yatabare
18 Sow
07 C Diarra
10 Maiga
15 Samassa

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.