Nigeria 1 Zambia 0

Imebadilishwa: 25 Januari, 2013 - Saa 15:00 GMT

Mchezaji wa Zambia wakati wa mechi yao na Ethipia

Mechi kati ya miamba wawili wa soka barani Afrika Nigeria na Zambia inaendelea .

Mechi hiyo inakisiwa kuwa moja ya mechi ngumu zaidi katika hatua ya makundi ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Afrika Kusini.

Kunako dakika ya 25,mlinda lango wa Zambia Davies Nkausu alimfanyia madhambi mshambulizi wa Nigeria Ahmed Musa na hivyo refa wa mechi hiyo kutoa penalti kwa Nigeria.

Lakini mcheza kiungo wake ambaye pia anaichezea klabu ya Chelsea akapoteza penalti hiyo na hivyo kuwapa mabingwa hao watetezi nafasi nyingine ya kupumua.

Katika kipindi hicho cha kwanza timu hizo mbili zilionekana kutoshana nguvu huku pande zote zikifanya mashambulio ya mara kwa mara.

Kufikia wakati wa mapunziko, hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwezio.

Nigeria ilianza kipindi cha pili kwa kasi zaidi na kufanya mashambulio kadhaa katika lango la Chipolopolo.

Na baada ya kupoteza mkwaju wa penalti John Obi Mikel, alijiimarisha zaidi kipindi cha pili na kunako dakika ya 56 Nigeria ikapata bao lake la kwanza .

Timu hizo mbili zilitoka sare katika mechi zao za ufunguzi.

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan, amewaandikia wachezaji wa Super Eagles na kuwapa ushauri wa jinsi ya kucheza mechi hiyo.

Kocha wa Nigeria, Stephen Keshi, vile vile alifika mbele ya viongozi wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Nigeria, kuelezea kwa nini hawakushinda mechi yao ya ufunguzi.

Mechi hiyo inayochezwa mjini Port Elizabeth ni muhimu sana katika harakati za timu hizo mbili kufuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.

Zambia ni bingwa mtetezi wa mashindano hayo, baada ya kuishinda Ivory Coast kwenye fainali za mwaka uliopita.

Maelezo zaidi kadri mechi inavyoendelea

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.