Algeria 0 Togo 1

Imebadilishwa: 26 Januari, 2013 - Saa 19:09 GMT

Togo inaongoza katika mechi yake dhidi ya Algeria kwa kufunga goli 1 kwa 0, ukiwa ni mchezo wa pili wa kundi D.

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Togo

Mshambuliaji Emmanuel Adebayor ndiye aliyeifungia timu yake bao muhimu katika kusaka nafasi ya kucheza robo fainali.

Awali kocha wa Algeria, Vahid Halilhodzic, alisema atafanya mabadiliko kadhaa katika kikosi chake kitakachopambana na Togo, katika mechi yao ya pili ya michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Afrika Kusini ili kuimarisha matumaini yao ya kufuzu kwa hatua ya robo fainali.

Magwiji hao kutoka Magharibi mwa Afrika nao wanahitaji ushindi katika mechi ya leo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupiga hatua, katika mashindano hayo.

Togo ilipoteza mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Ivory Coast kwa kufungwa magoli 2-1, huku nayo Algeria ikipoteza mechi yake ya kwanza kwa kucharazwa na Tunisia goli 1-0.

Mchezo wa kwanza wa kundi D umemalizika kwa Ivory Coast kuibuka washindi dhidi ya Tunisia kwa magoli 3-0.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.