Cape Verde yafuzu wa robo fainali ya AFCON

Imebadilishwa: 27 Januari, 2013 - Saa 18:57 GMT

Timu ya taifa ya Cape Verde

Cape Verde imeandikisha historia nyingine kwa kufuzu kwa robo fainali ya michuano ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika baada ya kuibanjua Angola kwa magoli mawili kwa moja.

Cape Verde ambayo inashiriki katika fainali hizo kwa mara ya kwanza ilitoka nyuma ya kufungwa bao moja kwa bila na Angola na kuandikisha ushindi wao wa kwanza katika fainali hizo.

Cape imemaliza na alama tano sawa na Afrika Kusini lakini ikizidiwa na wingi wa magoli.

Mshambulizi wa ziada Heldon, ndiye aliyeifungia Cape Verde bao lake la ushindi kunako dakika ya tisini ya mechi hiyo.

Angole ndio iliyokuwa ya kwanza kufunga kunako dakika ya 36 baada ya mchezaji wa Cape Verde kujifunga mwenyewe.

Mashabiki wa Angola

lakini vijana hao wa cape Verde walisawazisha kunako dakika ya 81 kupitia kwa mshambuliaji wake Varel.

Morocco nayo imeyaaga mashindano hayo katika raundi ya makundi sawia na Angola ambayo ilizoa alama mbili na moja mtawalia.

Kinyume na ilivyokuwa katika mechi kati ya Afrika Kusini na Morocco ni mashambiki wachache sana walihudhuria mechi hiyo na ushindi wa Afrika Kusini katika mechi yao ya mwisho huenda ukachochea mashabiki zaidi kufika katika viwanja mbali mbali wakati wa mechi ya robo fainali.

Cape Verde sasa inajumuika na Afrika Kusini na Ivory Cost ambayo tayari zimejikatia tikiti ya robo fainali ya mashindano hayo, yanayoendekea nchini Afrika Kusini.

Wawakilishi wa kanda ya Afrika Mashariki na Kati Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, kesho inajitosa uwanjani kucheza mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya Mali, mechi ambayo ni sharti washinde ili wafuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.