Ghana 2 Mali 0

Imebadilishwa: 28 Januari, 2013 - Saa 17:25 GMT
Timu ya soka ya Ghana

Mechi za mwisho za kundi B za hatua ya makundi zinechezwa leo nchini Afrika Kusini, huku michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika ikiendelea kupamba moto.

Ghana inachuana na Niger nayo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo inapepetana na Mali.

Ghana ilipata bao lake la kwanza kupitia kwa nyota wake Asamoah Gyan kunako dakika ya sita.

Niger ilijibu dakika mbili baadaye lakini bao hilo likakataliwa na refa wa mechi hiyo ambaye alisema kuwa washambuliajai wa Niger walimsukuma mlinda lango wa Ghana.

Kunako dakika ya 22, Ghana ikafunga bao lake la pili.

Kufikia sasa Ghana 2 Niger 0

Ghana inaongoza kundi hilo na alama nne na inahitaji sare ya aina yoyote ili ifuzu kwa hatua ya robo fainali.

Mali nayo inahitaji sare ya ili ifuzu ila mshindi wa pili katika kundi hilo huenda akaamuliwa kwa idadi ya magoli.

Wawakilishi wa pekee wa kanda ya Afrika mashariki na kati, katika mashindano hayo, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni sharti ishinde mechi ya leo ili ifuzu kwa robo fainali.

Kufikia sasa congo ina alama mbili pekee baada ya kutoka sare mechi zake mbili za kwanza.

Wenyeji wa mashindano hayo Afrika Kusini na Cape Verde wamefuzu kwa robo fainali katika kundi A nayo Ivoru Coast imejikatia tikiti ya robo fainali katika kundi D, baada ya kushinda mechi zake mbili za kwanza.

Vikosi

Niger Kikosi cha Ghana

Daouda,

Bachard,

Dankwa,

Chicoto,

Kourouma,

Koudize,

Soumaila,

Lancina,

Talatou,

Maazou,

Sidibe.

Wachezaji wa ziada

Alzouma,

Kader,

James,

Laouali,

Kamilou,

Dante,

Sakou,

Boubacar,

Alassane,

William,

Moutari.

Dauda,

Pantsil,

Boye,

Vorsah,

Afful,

Agyemang-Badu,

Rabiu,

Adomah,

Asamoah,

Atsu,

Gyan.

Wachezaji wa akiba

Agyei,

Richard Boateng,

Awal,

Annan,

Derek Boateng,

Akaminko,

Asante,

Clottey,

Boakye,

Mensah,

Kwarasey.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.