Ghana 3 Mali 0

Imebadilishwa: 28 Januari, 2013 - Saa 19:05 GMT
Timu ya soka ya Ghana

Ghana imefuzu kwa robo fainali ya michuano ya kuwania kombe la Mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Afrika.

Ghana imeilaza Niger magoli matatu kwa bila katika mechi yao ya mwisho ya Kundi B.

Ghana ilipata bao lake la kwanza kupitia kwa mcheza kiungo Asamoah Gyan kunako dakika ya sita.

Niger nayo ikajibu dakika mbili baadaye lakini bao hilo likakataliwa na refa wa mechi hiyo ambaye alisema kuwa washambuliajai wa Niger walimsukuma mlinda lango wa Ghana.

Kunako dakika ya 22, Christian Atsu naye akafunga bao la pili na kuiweka Ghana katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa robo fainali.

Timu hizo zilionekana nguzu huku pande zote zikifanya mashambulio ya mara kwa mara lakini kufikia wakati wa mapunziko matumaini ya Niger ya kufunga bao yalitumbukia nyongo na Ghana ilikuwa bado kifua mbele kwa magoli mawili kwa yai.

Muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza wachezaji wa Ghana, walididimiza matumaini ya Niger, kwa kufunga bao la tatu kupitia kwa nyota wake John Boye.

Ghana imefuzu kwa robo fainali hizo kwa kuzoa jumla ya alama saba baada ya kushinda mechi mbili na kutoka sare moja.

Katika kundi hilo hilo Mali imefuzu baada ya kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuzoa alama nne.

DRC ilimaliza katika nafasi ya tatu katika kundi hilo na alama tatu huku Niger ikizoa alama moja pekee.

Ghana, Mali, Afrika Kusini, Cape Verde na Ivory Coast ndizo timu ambazo tayri zimefuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.